Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum imetoa taarifa maalumu ya kupongeza mazishi ya kihistoria ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyofanywa na wananchi wakubwa na wenye heshima wa Iraq.
Katika sehemu ya taarifa hiyo imeelezwa kuwa: Mazishi haya makubwa yalikuwa ni hatua iliyoongeza nguvu na uwezo wa Umma wa Kiislamu, na Iraq ya wapambanaji imedhihirisha kuwa ni taifa kubwa, lenye heshima, lenye ustaarabu, lenye azma na irada thabiti, na kwamba litatekeleza nafasi yenye athari kubwa na ya kihistoria katika kuibuka kwa ustaarabu mpya wa Kiislamu.
Matini kamili ya ujumbe wa shukrani wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum kwa taifa kubwa la Iraq kutokana na mazishi ya kihistoria ya Imam Shahidi ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu
Sherehe za kuaga na mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Imam Shahidi Sayyid Ali Husseini Khamenei (ra), zimefanyika kwa utukufu mkubwa na adhama isiyo na kifani. Miongoni mwa matukio hayo, yale yaliyoshuhudiwa nchini Iraq na katika Miji Mitukufu ya Atabaat yalikuwa ni mandhari ya kipekee na yenye kugusa hisia, ambayo yameufanya ulimwengu kutambua kwa undani zaidi uhusiano wa karibu kati ya Iran na Iraq pamoja na nafasi ya Marjaiyya na utamaduni wa shahada mbele ya taifa la Iraq.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, kwa moyo wa dhati, inalishukuru taifa kubwa la Iraq, viongozi wa serikali ya Iraq, Hawza, wanazuoni watukufu na Mara'jii Wakuu wa Taqlid wa Iraq, hususan Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, ambao walionesha kiwango cha juu kabisa cha ukarimu na mapenzi.
Mazishi haya makubwa yalikuwa ni hatua iliyoongeza nguvu kwa Umma wa Kiislamu, na Iraq ya wapambanaji imedhihirisha kwamba ni taifa kubwa, lenye heshima, lenye utamaduni, lenye azma na irada thabiti, na litakuwa na nafasi yenye athari kubwa na ya kihistoria katika kuibuka kwa ustaarabu mpya wa Kiislamu.
Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum
Maoni yako